Rais Mahmoud Ahmadinejad amesema kuwa tauhidi, kupenda haki, kupigania uadilifu na amani, ni mingoni mwa sifa za taifa la Iran na kwamba sababu hiyo inawafanya maadui wapinge maendeleo ya Iran ya Kiislamu.Dakta Ahmadinejad ameyasema hayo leo katika kikao cha kwanza cha Umoja na Mshikamano wa Kitaifa wa Vijana wa Kiirani unaofanyika mjini Tehran. Rais wa Iran amebainisha namna uadui wa mfumo wa kibeberu ulivyoanzishwa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kueleza kuwa maadui daima wamekuwa wakigonga mwamba katika kutekeleza njama zao hizo dhidi ya wananchi wa Iran kutokana na utamaduni wenye nguvu wa taifa hili.Rais wa Iran pia ametoa mkono wa baraka na fanaka kwa Waislamu wote duniani kwa kuwadia Sikukuu ya Ghadir Khum na kueleza kuwa sikukuu hiyo ni idi kubwa ya mwanadamu na Mitume wote wa Mwenyezi Mungu.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 278323
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa sababu inayowafanya maadui wapinge ustawi wa Iran ya Kiislamu ni sifa ilizonazo nchi hii ya kupenda amani na kupigania haki na uadilifu.